Tuesday, 20 July 2021

MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)

 

MKATABA WA KUPANGISHA

CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)

 

BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA.

Ambaye katika mkataba huu atajulikana Kama mwenye nyumba- (Mpangishaji),

NA

NDUGU:……………………………………… S.L.P………………TANZANIA.

 Ambaye katika Mkataba huu atajulikana kama -(Mpangaji.)

 

 

Mpangaji amekubali kupanga kwa makubaliano haya yafuatayo:-

 

1. Kuanzia leo tarehe _____ mwezi _________ mwaka _________ hadi tarehe____________

2. Mpangaji atalipa kodi ya PANGO/CHUMBA Tsh._______________(kwa tarakimu)

__________________________________________________________( kwamaneno) .

Malipo ya Kodi yatalipwa kwa mkupuo mmoja wakati wa kuthibitisha.

 

3. Mpangishaji/Mwenye Nyumba  akishapokea fedha lazima atoe Stakabadhi kuonyesha amepokea fedha.

4.Gharama za kodi zinaweza kubadilika muda wowote kwa kupewa taarifa na Mpangishaji.

5. Kodi iliyokwishalipwa hairudishwi endapo utavunja Mkataba  mwenyeweMpangaji.

6. Mpangaji haruhusiwi kupangisha chumba alichokipanga au kumwachia mtu mwingine wakati wa mkataba wake bila ruhusa ya mwenye nyumba.

7. Mpangaji atatakiwa kutunza mazingira ya chumba na vitu vyote kwa wakati mmoja (usafi).

8. Marekebisho yoyote yanapaswa kupata kibali au baraka za mwenye Nyumba

9. Ifikapo mwisho wa mkataba mpangaji atakabidhi chumba husika kwa mwenye nyumba kikiwa katika hali ya usafi kama ulivyokabidhiwa wakati wakuingia.

10. Kama utaendelea na mkataba mpya utamjulisha mwenye nyumbana.Na  kama hauendelei pia utamjulisha mwenye nyumba.

MUHIMU:Chumba au nyumba ya biashara inapangishwa kwa mtu mwenye umri zaidi ya miaka 18,na pia azingatie sheria za nchi ikiwamo kuwa na vibali vya biashara kama TIN,Leseni Au Kitambulisho cha Ujasiriamali.

TAMKO (Mpangaji)

Mimi ………………………………Nikiwa na akili timamu nimeusoma mkabata huu na nimeelewa taratibu zote za mkataba huu na nimekubali kuzifuata kipindi chote cha mkataba wangu na nitakuwa tayari kuwajibika endapo nitavunja masharti au taratibu za mkataba huu.

 

KWA KUTHIBITISHA MKATABA huu kwa pande zote zinaweka sahihi zao kwa makubaliano yote yaliyoandikwa kwenye mkataba kwa hiari yao.

 

…………………………..                                              ……………………

Sahihi ya Mwenye Nyumba                                            Sahihi ya mpangaji

 

…………………………                                              …………………………

Jina kamili la mwenye nyumba                                     Jina kamili la Mpangaji          

SIMU Na………………………                                   SIMU Na……………………

TAREHE:…………………..                                        TAREHE:………………….


No comments:

Post a Comment

MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)

  MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)   BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...