Showing posts with label Imetayarishwa na Mwl.Albert J.Safari 0715803005. Show all posts
Showing posts with label Imetayarishwa na Mwl.Albert J.Safari 0715803005. Show all posts

Sunday, 8 April 2018

ALOMOFU

Alomofu (kutoka Kiingereza "allomorph") ni msamiati uliotumika kwanza kuelezea mabadiliko ya
muundo wa kikemia. Mwaka 1948 Fatih Şat na Sibel Merve walianza kuutumia upande wa lugha katika kitabu chao Language XXIV.

Dhana yake
Dhana ya alomofu ni dhana inayojadiliwa katika isimu ya lugha.

Dhana hii hujadiliwa sana katika
mofolojia ya lugha yaani, sarufi maumbo .

Kimsingi huwezi kupata dhana kamili na inayoeleweka kama huwezi kuhusianisha alomofu na
mofimu. Ndiyo maana fasili ya alomofu kwa maana ya kikamusi inaweza kuwa:

1. Umbo jingine la mofimu ileile
2. Aina mbalimbali za mofimu moja

Ukiangalia maana hizo mbili za neno alomofu utabaini uhusiano wa neno hilo na mofimu. Yaani huwezi kutaja Alomofu kama huwezi kuhusisha mofimu.

Kwa ujumla, kilugha, dhana ya alomofu huweza kufasirika kama: "Maumbo zaidi ya moja yanayowakilisha mofimu moja kisarufi". Kwa mujibu wa
wanaisimu neno hili limegawanyika kama ifuatavyo:

ALO = Zaidi ya moja
MOFU = Ni kipashio cha kimofolojia kiwakilishacho mofimu.

Mofu ni umbo ambalo huweza kuandikwa watu wanapoandika maneno, pia huweza kutamkwa watu wanapotamka maneno.
Tazama mfano wa maneno yafuatayo:

Mtoto = Neno hili lina mofu mbili, ambazo ni M - toto

Analima = Neno hili lina mofu tatu , ambazo ni: A- na - lim - a

Baba = Neno hili lina mofu moja ambayo ni: Baba

Kumbuka: baadhi ya wanaisimu wanaamini kuwa hata mzizi wa neno ni mofu pia.

Namna ya kuzitambua alomofu
Ukirejea katika mofimu, utakuta mofimu huweza kufanya kazi tofauti katika neno.

Mofimu huweza kudokeza
nafsi , wakati, umoja au wingi wa
nomino na hata kauli mbalimbali za
kitenzi .

Mfano:
Anacheza = A-na-chez-a
Tuliondoka = Tu -li-ondok-a
Wanaita = Wa -na-it-a

Katika mfano huo, mofimu zilizokozwa
wino ni mofimu zinazodokeza nafsi. Kwa hiyo, tunapopata mofimu tofauti, yaani zenye maumbo tofauti lakini zinafanya kazi moja kisarufi huitwa ALOMOFU. Kwa mfano huo, hapo A, Tu na Wa tutaziita ni Alomofu za nafsi.
Tazama mfano wa pili:

Mtoto = M -toto,
Watoto = Wa -toto,
Mwalimu = Mw -alimu

Katika mfano huo, maneno yaliyokozwa wino ambayo ni M , Wa na Mw ni mofimu zinazodokeza umoja na wingi wa nomino. Kwa kuwa maumbo ya mofimu hizo ni tofauti lakini hufanya kazi moja kisarufi, ndiyo maana tunaziita Alomofu.

Mazingira yanayosababisha kutokea kwa alomofu:

Alomofu hutokana na mazingira tofautitofauti.

Alomofu zinaweza kutokana na mazingira yafuatayo:

Kifonolojia
Hapa tunaweza kuona mifano ya mazingira yanayoweza kutokea kwa mofimu na alomofu zake katika
unyambulishaji wa vitenzi vya Kiswahili .

Mfano: Kutendeka
Piga -               Pig- ik-a
Cheza -            Chez- ek -a
Zoa -                 Zo- lek-a
Chukua -           Chuku- lik -a

Hapo mofimu ik inayobainisha dhana ya kutendeka ina Alomofu nne , ambazo ni: Ik, ek, lek na lik

Kileksika
Hapa tunaweza kuona mofimu na alomofu zake katika ngeli za majina. Kwa mfano, katika ngeli ya kwanza na ya pili yaani, m/wa

Mfano
M -tu -                   wa -tu
M -ke -                   wa -ke
Mw -alimu -           wa -alimu
Mu -uguzi -             wa -uguzi

Katika mfano huo, tunaona mofimu m yenye dhana ya umoja ina alomofu tatu ambazo ni: M , Mw na Mu.

Kisarufi
Hapa tunapata mofimu na alomofu zake katika mofimu ya njeo (wakati).

Mofimu ya nje inawakilishwa na alomofu zifuatazo:
A- na -pika = Wakati uliopo
A- li -pika = Wakati uliopita
A- ta -pika = Wakati ujao

Hapo alomofu za njeo ni: na , li , na ta

DHANA YA MOFU

DHANA YA MOFU
Mofu ni umbo kietimolojia
Mofimu ni maana (kabla ya kuja kwa sarufi mamboleo neno mofimu lilitumika kwa maana ya umbo na maana, dhana hii ilianzishwa na mtaalamu wa Isimu aitwaye Noam homsky lakini baadaye ikaamuliwa kuwa Mofimu itumike kuukilia maana kwa sababu kietimolojia mofimu hmaanisha maana – elementi dhahania.
Alo = zaidi ya moja (mf. Alomofu = maumbo zaidi ya moja yanayowakilisha mofimu (maana) moja kisarufi).
NB: Maana ya kietimolojia ni fasili ya neno au kitu kutoka kwenye lugha yake ya asili.

MOFU
Ni kipashio cha kimofolojia kinachosetiri mofimu (maana).

Mofu ni umbo ambalo huweza kuandikwa watu wanapoandika maneno na pia huweza kutamkwa watu wanapotamka maneno.

Kwa hiyo neno lolote lenye maana sharti liwe na mofu angalau moja kwa msingi kwamba maana ni elementi dhahania ambayo hubebwa na umbo fulani.

AINA ZA MOFU
Mofu huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili ambavyo ni:

Maana inayobebwa na mofu na
Mofolojia ya mofu.

Aina za mofu kwa kigezo cha maana
Kigezo hiki kina aina tatu za mofu ambazo ni mofu huru, mofu funge na mofu tata

1.Mofu huru
Hizi ni mofu ambazo husimama kama maneno kamili yanayojitosheleza kimuundo na kitaarifa.
mf. Baba, mama, safi, Sali, kaka, n.k

2.Mofu funge/tegemezi
Ni vijisehemu vya neno vinavyojiegemeza kwenye mzizi wa neno ili kutoa taarifa fulani. Kila kipande cha neno ni mofu funge.
mf.
Anaimba = A-na-imb-a
Tuliochezeana = Tu-li-o-chez-ean-a

3.Mofu Tata
Hizi ni mofu ambazo zikitumiwa katika maneno huleta utata, hufanya neno liwe na maana zaidi ya moja.
Mf:
Juma aliwacheze a wanangu
Katika tungo hiyo kuna utata wa kimaana ambao unabebwa na neno
aliwachezea . Kimsingi utata katika neno hilo unasababishwa na kauli ya kutendea ambayo imebebwa na mofu –e- ya utendea. Maana zinazoletwa na mofu hiyo ya utendea ni kuwa ukisema Juma aliwachezea wanangu
wanaokusikiliza wanaweza kuelewa kuwa:
(i) Juma alicheza ili kuwafurahisha watoto
(ii) Juma alicheza kwa niaba ya watoto
(iii) Juma aliwaroga watoto
(iv) Juma aliwafanyia watoto tendo la udhalilishaji
Maana zote hizo zinaletwa na mofu – e- na hiyo ndio tunaiita mofu tata.

Aina za mofu kwa kigezo cha mofolojia
Hapa tunapata aina mbili za mofu za mofu ambazo ni mofu changamano na mofu kapa

4.Mofu Changamano
Mofu changamano huundwa kwa kuweka pamoja mzizi au shina zaidi ya moja ili kuunda neno moja. Katika hali ya kawaida kila moja ya mizizi hiyo huweza kusimama peke yake na kuunda neno lake.
Mf.
Mwana + nchi
Mwana + chama
Askari + kanzu

5.Mofu Kapa
Ni maumbo ambayo hayadhihiriki kimatamshi (kifonolojia) wala kimaandishi (kiothografia) lakini athari zake zipo akilini mwa wazungumzaji. Katika maandishi mofu hizi huwakilishwa na msimbo (alama) θ. Katika Kiswahili kuna mofu kapa za umoja na za wingi.
mf. 1
Umoja
Wingi
θ+sanduku ma+sanduku
θ+debe ma+debe
θ+chungwa ma+chungwa
mf. 2
Umoja wingi
U+nywele θ+nywele
U+kucha θ+kucha
U+funguo θ+funguo
Katika mfano wa kwanza (1) hakuna mofu za umoja lakini za wingi zipo na katika mfano wa pili (2) mofu za umoja zipo na za wingi hazipo. Kwa hiyo mtu akisema “ …niletee sanduku ” inajulikana ni sanduku moja na akisema, “ …niletee masanduku” inajulikana ni zaidi ya moja. Hali kadhalika ukiambiwa funguo ni tofauti na ukiambiwa ufunguo. Mofu kapa huwa akilini mwa wasemaji wa lugha.

MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)

  MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)   BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...