Sunday, 8 April 2018

DHANA YA MOFU

DHANA YA MOFU
Mofu ni umbo kietimolojia
Mofimu ni maana (kabla ya kuja kwa sarufi mamboleo neno mofimu lilitumika kwa maana ya umbo na maana, dhana hii ilianzishwa na mtaalamu wa Isimu aitwaye Noam homsky lakini baadaye ikaamuliwa kuwa Mofimu itumike kuukilia maana kwa sababu kietimolojia mofimu hmaanisha maana – elementi dhahania.
Alo = zaidi ya moja (mf. Alomofu = maumbo zaidi ya moja yanayowakilisha mofimu (maana) moja kisarufi).
NB: Maana ya kietimolojia ni fasili ya neno au kitu kutoka kwenye lugha yake ya asili.

MOFU
Ni kipashio cha kimofolojia kinachosetiri mofimu (maana).

Mofu ni umbo ambalo huweza kuandikwa watu wanapoandika maneno na pia huweza kutamkwa watu wanapotamka maneno.

Kwa hiyo neno lolote lenye maana sharti liwe na mofu angalau moja kwa msingi kwamba maana ni elementi dhahania ambayo hubebwa na umbo fulani.

AINA ZA MOFU
Mofu huainishwa kwa kuzingatia vigezo viwili ambavyo ni:

Maana inayobebwa na mofu na
Mofolojia ya mofu.

Aina za mofu kwa kigezo cha maana
Kigezo hiki kina aina tatu za mofu ambazo ni mofu huru, mofu funge na mofu tata

1.Mofu huru
Hizi ni mofu ambazo husimama kama maneno kamili yanayojitosheleza kimuundo na kitaarifa.
mf. Baba, mama, safi, Sali, kaka, n.k

2.Mofu funge/tegemezi
Ni vijisehemu vya neno vinavyojiegemeza kwenye mzizi wa neno ili kutoa taarifa fulani. Kila kipande cha neno ni mofu funge.
mf.
Anaimba = A-na-imb-a
Tuliochezeana = Tu-li-o-chez-ean-a

3.Mofu Tata
Hizi ni mofu ambazo zikitumiwa katika maneno huleta utata, hufanya neno liwe na maana zaidi ya moja.
Mf:
Juma aliwacheze a wanangu
Katika tungo hiyo kuna utata wa kimaana ambao unabebwa na neno
aliwachezea . Kimsingi utata katika neno hilo unasababishwa na kauli ya kutendea ambayo imebebwa na mofu –e- ya utendea. Maana zinazoletwa na mofu hiyo ya utendea ni kuwa ukisema Juma aliwachezea wanangu
wanaokusikiliza wanaweza kuelewa kuwa:
(i) Juma alicheza ili kuwafurahisha watoto
(ii) Juma alicheza kwa niaba ya watoto
(iii) Juma aliwaroga watoto
(iv) Juma aliwafanyia watoto tendo la udhalilishaji
Maana zote hizo zinaletwa na mofu – e- na hiyo ndio tunaiita mofu tata.

Aina za mofu kwa kigezo cha mofolojia
Hapa tunapata aina mbili za mofu za mofu ambazo ni mofu changamano na mofu kapa

4.Mofu Changamano
Mofu changamano huundwa kwa kuweka pamoja mzizi au shina zaidi ya moja ili kuunda neno moja. Katika hali ya kawaida kila moja ya mizizi hiyo huweza kusimama peke yake na kuunda neno lake.
Mf.
Mwana + nchi
Mwana + chama
Askari + kanzu

5.Mofu Kapa
Ni maumbo ambayo hayadhihiriki kimatamshi (kifonolojia) wala kimaandishi (kiothografia) lakini athari zake zipo akilini mwa wazungumzaji. Katika maandishi mofu hizi huwakilishwa na msimbo (alama) θ. Katika Kiswahili kuna mofu kapa za umoja na za wingi.
mf. 1
Umoja
Wingi
θ+sanduku ma+sanduku
θ+debe ma+debe
θ+chungwa ma+chungwa
mf. 2
Umoja wingi
U+nywele θ+nywele
U+kucha θ+kucha
U+funguo θ+funguo
Katika mfano wa kwanza (1) hakuna mofu za umoja lakini za wingi zipo na katika mfano wa pili (2) mofu za umoja zipo na za wingi hazipo. Kwa hiyo mtu akisema “ …niletee sanduku ” inajulikana ni sanduku moja na akisema, “ …niletee masanduku” inajulikana ni zaidi ya moja. Hali kadhalika ukiambiwa funguo ni tofauti na ukiambiwa ufunguo. Mofu kapa huwa akilini mwa wasemaji wa lugha.

No comments:

Post a Comment

MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)

  MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)   BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...