SILABI ZA KISWAHILI
Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi funge na silabi huru.
Silabi huru ni zile ambazo huishia na irabu.
Kwa mfano; la, ma, kwa, mba, n.k.
Silabi funge ni zile zinazoishia na konsonanti ambapo katika lugha ya Kiswahili ni nadra kuzipata maana lugha hii inatumia silabi huru lakini hupatikana katika maneno ya Kiswahili yanayokopwa kutoka katika lugha nyingine.
Kwa mfano; Alhamisi – a-l-ha-mi-si
Taksi - ta-k-si
Miundo ya Silabi za Kiswahili
a. Muundo wa irabu peke yake (I) - Yapo maneno katika lugha ya Kiswahili yanayoundwa na irabu peke yake kama silabi. Mfano; u+a = Ua, o+a = Oa, a+u = Au, n.k.
b. Muundo wakonsonanti pekee (K) – Kiswahili hakina maneno mengi yanayoundwa na silabi pekee isipokuwa maneno machache ambayo huwa ni ya nazali /M/ na /N/ na huwa zinatumika ama mwanzoni au katikati ya neno. Mfano; m+ke =Mke, m+bwa = Mbwa, n+chi =Nchi n.k
c. Muundo wa konsonanti na irabu (KI) – Katika muundo huu konsonanti hutangulia irabu. Mfano; b+a = Ba, k+a = Ka n.k.
d. Muundo wa konsonanti mbili na irabu (KKI) – Katika muundo huukonsonanti mbili hutangulia irabu. Mara nyingi konsonanti ya pili huwa ni kiyeyusho. Mfano; k+w+a = Kwa, m+w+a = Mwa, b+w+a = bwa, n+d+e = Nde, n.k.
e. Muundo wa konsonanti tatu na irabu (KKKI) – Muundo wa namna hii hujitokeza katika maneno machache. Mfano; Bambwa, Tingwa, Tindwa,Mbwa, n.k.
f. Muundo wa silabi funge – Huu hujitokeza katika maneno machache ambayo huwa ya mkopo. Mfano; Il-ha-li = Ilhali,Lab-da = Labda
No comments:
Post a Comment