KOZI: MATUMIZI YA SARUFI
MADA : DHANA YA ALOMOFU
MWL.ALBERTO SAFARI
SIMU: 0715803005
BARUA PEPE: salbertode@yahoo.com
ALOMOFU
Alomofu ni neno ambalo linatokana na maneno mawili ambayo ni ALO na MOFU
yenye maana zaidi ya moja na umbo.Kwa hiyo tunapozungumzia alomofu tunamaanisha
maumbo zaidi ya moja/mbalimbali yanayowakilisha mofimu(maana) moja kisarufi.
Alomofu ni vivuli au vipashio au maumbo mbalimbali, yaani {alo},
yanayowakilisha kitu fulani; hapa kitu chenyewe ni mofu.Jumla yavivuli au maumbo
husika, husetiri maana moja ya mofu husika, lakini vivuli hivi havina uwezo wa
kubadilisha maana ya mofu husika.
ALOMOFU ZA
|
||||
WAKATI
|
NAFSI
|
UREJESHI
|
UKANUSHI
|
UTENDESHI
|
LI
KU
NA
TA
|
NI
TU
U
M
A
WA
|
YE
O
CHO
VYO
YO
LO
PO
MO
KO
|
SI
HA/HU
HA
|
ISH
ESH
LISH
LESH
Z
|
Jedwali
la hapo juu linaonesha baadhi tu ya alomofu za Kiswahili lakini zipo alomofu
nyingi mbalimbali.Kumbuka kuwa alomofu ni maumbo mbalimbali yayowakilisha
mofimu moja kisarufi
Aina za Alomofu
(i) Alomofu za Mofu Zenye
Maana ya Nafsi
Alomofu za Mofu ya Nafsizinajitokeza katika hali ya umojana wingi kama
ifuatavyo:
Alomofu za Mofu ya Nafsi katika hali ya umoja ni:
Nafsi ya kwanza (mzungumzaji): {ni};
nafsi ya pili(unayempasha habari): {u};]
Nafsi ya tatu (habari yenyewe), kama ni mtu, alomofu yake ni {a},
na kama ni kitu, alomofu yake ni {ki}
ambayo nayo itajibainisha kwa mujibu
wa ngeli ya kila kitu husika katika mazungumzo kati ya nafsi ya kwanza na ya
pili.
Alomofu za Mofu ya Nafsi katika hali ya wingi ni:
Nafsi ya kwanza (mzungumzaji): {tu;
Nafsi ya pili (unayempasha habari): {m}
Nafsi ya tatu (habari yenyewe), kama ni mtu,
alomofu yake ni {wa},na kama ni kitu, alomofu yake ni {vi} ambayo nayo itajibainisha kwa mujibu wa ngeli ya kila kitu
husika katika mazungumzo kati ya nafsi ya kwanza na ya pili.
(ii) Alomofu za Mofu Zenye
Maana ya Njeo
Baadhi ya Alomofu zinazowakilisha mofu ya njeo sambamba na njeo husika ni:
MOFU YA
NJEO
|
ALOMOFU
|
NJEO
|
{-na-}
|
iliyopo
|
|
{-li-}
|
iliyopita
|
|
{-ta-}
|
ijayo
|
(iii) Alomofu za Mofu ya Masharti/Kutegemeana/Shurutia
Mofu ya masharti/kutegemeana/shurutia inaweza kuwakilishwa na alomofu,
yaani maumbile/vivuli mbalimbali vya mofu ya masharti/kutegemeana. Ni mofu ya
masharti au kutegemeana kwa sababu jambo mojawapo kati ya mawili yanayotakiwa
lazima liwepo ndipo jambo la pili lifanyike, vinginevyo, mambo hayafanyiki.
Mfano:
Alomofu {-ki-}, {-nge-}, {-ngali-}, [-japo-}, {endapo}, nk. katika:
Bwana Nihuka akija ICE, atakutana na Dakta Nchimbi.
Bwana Nihuka angekuja ICE, angekutana
na Dakta Nchimbi.
Endapo Bwana Nihuka atakuja ICE, atakutana na Dakta
Nchimbi.
Bwana Nihuka angalikuja ICE,
angalikutana na Dakta Nchimbi.
Ajapo
Bwana Nihuka ICE, atakutana na Dakta Nchimbi.
Ilivyo hapa ni kwamba {-ki-}, {-nge-}, {-ngali-}, [-japo-}, {endapo}
zote ni alomofu ambazo zinasetiri maana ya mofu moja ambayo ni ya mashariti; ni
mofu ya mashariti kwa sababu Bwana Nihuka hawezi kukutana na Dakta Nchimbi
mpaka hapo atakapokwenda ICE. Kwa maana nyingine, kukutana kwa Bwana Nihuka na
Dakta Nchimbi kunategemea kitendo cha Dakta Nchimbi kuwepo ICE na Bwana Nihuka
kwenda hapo ICE.
(iv) Alomofu za Mofu ya
Kutendea {i}
Mofu ya Kutendea {i}inaweza kuwakilishwa na alomofu nne zinazojitokeza
katika mazingira kifonolojia wakati wa unyambulishaji wa mofu za vitenzi vyenye
asili ya Kiswahili; nazo ni {i}, {e},
{li}, {le}.
(a) Alomofu
{i} ya Mofu ya Kutendea {i}hutokea iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na
konsonanti katika mzizi ambao una irabu ama /a/, au /i/, au /u/; kwa
mfano:
paka => {pak}
+ {a} => pakia => {pak} + {i} + [a}.
kata
=> {kat} + {a} => katia => {kat} + {i}
+ [a}.
lima => {lim}
+ {a} => limia => {lim} + {i} + [a}.
zima
=> {zim} + {a} => zimia => {zim} + {i} + [a}.
funga => {fung}
+ {a} => fungia => {fung} + {i} + [a}.
suka
=> {suk} + {a} => sukia => {suk} + {i} + [a}
nk.
(b) Alomofu
{e} ya Mofu ya Kutendea {i}hutokea iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na
konsonanti katika mzizi ambao una irabu ama /e/, au /o/; kwa mfano:
teka
=> {tek} + {a} => tekea => {tek} + {e} + [a}.
tenda
=> {tend} + {a} => tendea => {tend} + {e} + [a}.
toka
=> {tok} + {a} => tokea => {tok} + {e} + [a}.
soma
=> {som} + {a} => somea => {som} + {e} + [a}.
nk.
(c) Alomofu
{le} ya Mofu ya Kutendea {i}hutokea iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na
irabu ama /e/, au /o/; kwa mfano:
zoa
=> {zo} + {a} => zolea =>
{zo} + {le} + [a}.
toa
=> {to} + {a} => tolea => {to} + {le} + [a}.
nk.
(d) Alomofu
{li} ya Mofu ya Kutendea {i}hutokea iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na
irabu ama /a/ /i/ au /u/.; kwa mfano:
kaa
=> {ka} + {a} => kalia => {ka} + {li} + [a}
zaa
=> {za} + {a} => zalia => {za} + {li} + [a}
kimbia
=> {kimbi} + {a} => kimbilia => {kimbi} + {li} + [a}
tia
=> {ti} + {a} => tilia => {ti} + {li} + [a}
pakua
=> {paku} + {a} => pakulia => {paku} + {li} + [a}
tua
=> {tu} + {a} => tulia => {tu} + {li} + [a}
(v) Alomofu za Mofu ya Kutendeka {ek}
Mofu ya Kutendeka {ek}inaweza kuwakilishwa na alomofu nnezinazojitokeza
katika mazingira kifonolojia wakati wa unyambulishaji wa
mofu za vitenzi vyenye asili ya
Kiswahili; nazo ni {ik},{ek},{lik} na {lek}.
(a) Alomofu
{ek} ya Mofu ya Kutendea {ek}hutokea iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na
konsonanti katika mzizi ambao una irabu /e/; kwa mfano:
penya
=> {peny} + {a} => penyeka
=> {peny} + {ek} + [a}.
sema
=> {sem} + {a} => semeka =>
{sem} + {ek} + [a}.
(b) Alomofu {ik} ya Mofu ya Kutendea {ik}hutokea
iwapo mzizi wa kitenzi
unaishia na konsonanti na ambao una irabu /a/,/i/,/na/,/u/ kwa mfano:
kata
=> {kat} + {a} => katika => {kat} + {ik} + [a}.
lamba
=> {lamb} + {a} => lambika => {lamb} + {ik} + [a}
pika
=> (pik) + (a) =>
pikika
vuta
=> (vut) + (a) => vutika
(c) Alomofu {lek} ya Mofu ya Kutendea {ek}hutokea
iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na irabu /o/; kwa mfano:
toboa=>
{tobo} + {a} => toboleka =>
{tobo} + {lek} + [a}.
zoa
=> {zo} + {a} => zoleka =>
{zo} + {lek} + {a}.
(d) Alomofu {lik} ya Mofu ya Kutendea {ek}hutokea
iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na irabu /u/; kwa mfano:
chukua=>
{chuku} + {a} => chukulika =>
{chuku} + {lik} + [a}.
sahau=>
{sahau} => sahaulika =>
{sahau} + {lik} + [a}.
(vi) Alomofu za Mofu ya
Kutendesha {esh}
Mofu ya Kutendesha {esh}inaweza kuwakilishwa na alomofutano zinazojitokeza katika mazingira kifonolojia wakati wa
unyambulishaji wa mofu za vitenzi vyenye asili ya Kiswahili; nazo ni
{ish},{esh}, {iz}, {lish} na {lesh.
(a)
Alomofu {esh} ya Mofu ya Kutendesha {esh}hutokea
iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na konsonanti katika mzizi ambao una irabu /e/.
au /o/; kwa mfano:
weza=> {wez} + {a}
=> wezesha => {wez} + {esh} + [a}.
enda => {end} + {a}
=> endesha => {end} + {esh} + [a}.
lewa => {lew} + {a} =>
lewesha => {lew} + {esh} + {a}
choka => {chok} +
{a} => chokesha => {chok} + {esh} + [a}.
koma => {kom} + {a}
=> komesha => {kom} + {esh} + [a}.
(b) Alomofu {ish} ya Mofu ya Kutendesha {esh}hutokea
iwapo mzizi wa kitenzi unaishia na konsonanti katika mzizi ambao una irabu /a/.
/i/, au /u/; kwa mfano:
kata
=> {kat} + {a} => katisha => {kat} + {ish} + [a}.
lamba => {lamb} + {a} => lambisha => {lamb} + {ish} + [a}.
lipa
=> {lip} + {a} => lipisha => {lip} + {ish} + {a}.
funda
=> {fund} + {a} => fundisha => {fund} + {ish} + {a}.
fumba => {fumb} + {a} => fumbisha => {fumb} + {ish} + {a}.
(vii) Alomofu {fy}, {vy}, {sh},
{z} ya Mofu ya Kutendesha {esh}
Utokeaji waalomofu {fy}, {vy},
{sh}, {z}ya Mofu ya Kutendesha {esh}
haufuati kanuni zinazotabirika; kwa mfano:
ogopa
=> {ogop} + {a} => ogofya =>
{ogo} + {fy} + [a}.
lewa
=> {lew} + {a} => levya =>
{le} + {vy} + [a} = lewesha
shuka
=> {shuk} + {a} => shusha
=> {shu} + {sh} + {a}
= shukisha.
Lala => laza
(viii) Alomofu {e}, {i} za Mofu
Tamatishi {a}
Ieleweke kwamba vitenzi asilia vyote katika Kiswahili huishia kwa
kiambishi [a], na kwa hiyo, kuitwa Kiambishi Tamati {a} ambacho kazi yake kubwa
kuyakinisha tendo linaloashiriwa na kitenzi husika katika hatua yake ya mwisho
ya matumizi katika sentensi. Kwa mantiki hiyo, kiambishi tamati hiki huitwa
Mofu Tamatishi {a}. Mofu tamatishi hii ina alomofu zake ambazo ni {e} na {i}.
(a) Alomofu {e} ya Mofu Tamatishi {a}
Alomofu {e} ya mofu tamatishi {a}, hutokea wakati mofu tamatishi {a}
inapoashiria tendo la kuiamrisha nafsi ya tatu,kwa mfano:
Kitenzi
|
Tendo la Kuiamrisha Nafsi ya Pili
|
Tendo la Kuiamrisha Nafsi ya Tatu
|
Kukimbi-a
|
kimbi-a
|
akimbi-e
|
Kulip-a
|
lip-a
|
Alip-e
|
nk.
(b) Alomofu {i} ya Mofu
Tamatishi {a}
Alomofu {i} ya mofu tamatishi {a}, hutokea wakati mofu tamatishi {a}
inapoashiria tendo la kukanusha ambalo hufanywa na nafsi zote tatu katika umoja na wingi wake, kwa mfano:
Tendo la Kuiamrisha Nafsi ya Pili
|
Kukanushwa kwa Tendo na Nafsi Zote Tatu – Umoja
|
Kukanushwa kwa Tendo na Nafsi Zote Tatu – Wingi
|
kimbi-a
|
Nafsi -1: sikimbi-i
Nafsi -2: hukimbi-i
Nafsi -3: hakimbi-i
|
Nafsi -1: hatukimbi-I
Nafsi -2: hamkimbi-i
Nafsi -3: hawakimbi-i
|
lip-a
|
Nafsi -1: silip-i
Nafsi -2: hulip-i
Nafsi -3: halipi-i
|
Nafsi -1: hatulip-I
Nafsi -2: hamlip-i
Nafsi -3: hawalipi-i
|
No comments:
Post a Comment