SUALA LA UTENDAJI KATIKA FASIHI SMULIZI
Katika fasihi simulizi utendaji ni uti wa mgongo yaani ni suala la msingi.
Mulokozi (1996:24) Fasihi simulizi ni tukio na linafungamana na matukio ya kijamii na hutawaliwa na fanani (msanii au mtendaji)
Ø Fanani ni mtendaji au mwasilishaji na mtunzi wa kipera,fani husika kwa hadhira katika muktadha wa tukio fulani ,kazi yake yaweza kuwa kichwani au akatunga papo kwa papo.
Ø Fani inayotendwa au kipera
Ø Hadhira/wasikilizaji,washiriki,wachangiaji ,wahakiki,watazamaji hawa huangalia uzuri au ubaya.
Ø Tukio-ni shughuli yoyote ya kijamii ambayo ndio muktadha wa utendaji.mfano msiba,ibada,harusi,sherehe,n.k
Ø Mahali –eneo mahsusi ambapo sanaa hiyo inatendwa.
Ø Wakati na muda maalum au majira maalum ya utendaji .Vipera vingi vina wakati wake.mfano Sifo huimbwa wakati wa kuomba.Mwingiliano huu wa vipengele hivi ndiyo unaoamua fani hiyo iwasilishwe vipi.
OKPEWHO (1992) Anasema Utendaji unaotofauta kutokana na sababu mbali mbali kama vile;
Ø Umri wa fanani
Ø Umri wa hadhira
Ø Nguvu ya fanani,baadhi ya vipera vinahitaji fanani awe na nguvu mfno majigambo
Ø Tukio husika mfano Msiba hauwezi kufanana na sherehe
Ø Aina ya mandhari au jukwaa maalum la kutendea yaani pale inapotendewa.
Ø Vifaa ambatani vinavyotumika na fanani katika utendaji mfano maleba,mkuki
Ø Idadi ya fanani
Pia utendaji unatokana au unatawaliwa na;
Ø Dhima ya kipera( tukio ),muktadha wa uwasilishaji na namna ya uwasilishaji hutegemea dhima ya kipera katika jamii.
Ø Muda na mahali,ni muhimu kuzingatia kwa kipera chochote hutegemea au husukumwa na muda na mahali.mfano matambiko yanafanywa muda gani?
Ø Mila na utamaduni ,kila jamii ina mila na utamaduni wake na hivyo huathiri utendaji wa vipera husika.mfano Mavazi au maleba maalum ya kisanaa yaani kipera hiki kinahitaji aina ipi ya maleba?
Ø Sifa za wahusika au watendaji wa kipera fulani wanapaswa wawe akina nani?
SWALI; JE UTENDAJI NI NINI?
Muluka (1999) anasema Utendaji ni uwasilishaji wa hadithi au ngano unaofanywa na msanii kwa hadhira kwa kutumia mdomo na kuambatana na matendo ya viungo mbalimbali vya mwili na ishara uso.Hivyo kila kipera kipo kwaajili ya kutendwa.
UTENDAJI KATIKA VIPERA MBALI MBALI
Finnegan (1970) ‘’ Oral Literature in Africa’’ anasema kuwa katika utendaji kuna kanuni maalum,jamii nyingi zina utamaduni wake.Hadithi ni utanzu muhimu katika jamii za kiafrika.Hadithi ni utanzu wa jioni na mtambaji anazungukwa na hadhira.
SWALI; Je kwanini hadithi inatambwa jioni?
Ø K wasababu mchana mtambaji anakuwa katika utafutaji yaani katika shughuli zake za kila siku.
Ø Hadithi ina fomula zake za kuanza na kumalizia yaani mianzo na miisho maalum ya kihadithi.
Ø Katika kutamba hadithi fanani habanwi kutumia vipera vingine katika utendaji wake.
Ø Katika kutamba hadithi msimuliaji hatakiwi kukalili ila anapaswa kuleta upya fulani wa utendaji wa hadithi hiyo.
Ø Mtambaji anapaswa kutumia sauti vizuri na iendane na utanzu wenyewe.
Ø Kuna wasimuliaji wazuri na wabaya au wasiowazuri
Ø Msimuliaji awe mbunifu ili kunogesha hadithi
Ø Katika utendaji msimuliaji aoneshe hisia zake.
UFALAGUZI
Ni uwezo alionao fanani katika kuunda kutunga ,kugeuza na kuiwasilisha kazi ya fasihi simulizi papo kwa papo bila ya kujifunga na muundo asilia au na muundo uliozoeleka. Hivyo katika utendaji wa kipera fulani kuna utungaji mpya kutokana na mbinu fulani unazotumia.
Ø Hivyo hadithi moja inaweza simuliwa tofauti na wasimuliaji tofauti.Utendaji wa kipera hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine.
SIFA ZA FANANI BORA
Senkoro anasema Fanani bora anatakiwa afanye kazi ya ualimu ,awe mtoa maoni,msanii,mburudishaji,muigizaji
Ø Fanani aifanye hadithi ionekane mpya kila mara anaposimulia.
Ø Fanani aifurahie na kujivunia fani anayoitenda,kuisimulia ipasavyo.
Ø Fanani awe mbunifu na awe na kumbukumbu.
Ø Suala la utamaduni katika utendaji fanani azingatie utamaduni wa kipera anachotamba.
Ø Fanani awe tajiri wa lugha yaani ajue kutumia mbinu mbalimbali za lugha kama vile nahau,semi,n.k.
Ø Fanani asiwe na aibu katika utendaji atumie vema lugha na viungo mbali mbali.
Ø Kujua mambo ya kihistoria kwani Fasihi inapitia vipindi mbalimbali.
UTENDAJI WA KIPERA CHA SEMI
1. METHALI
Ni usemi mfupi wa kimapokeo unaodokeza mafumbo mazito au fikra zinazotokana na uzoefu wa jamii husika.Katika utendaji unaweza kutofautiana na vipera vingine kwani utendaji wa methali lazima unajitegemeza wakati wa kutenda fani nyingine mfano mkutano,maongezi ya kawaida,majadiliano,hadithi,wakati wa kukanya mtu n.k.
Kimsingi watambaji wa methali ni watu wazima (wazee) kutokana na kuishi kwao katika jamii kwa muda mrefu.
2. VITENDAWILI
Utendaji katika vitendawili si tegemezi kama methali bali kitendawili kinasimama chenyewe kwa kufuata kanuni zilizowekwa na jamii husika.Mfano katika kabila la wajaluo ukishindwa kutegua unaombwa mke au mme na katika jamii nyingine unapewa mji.
2. MAJIGAMBO
Katika Jamii ya wahaya ni jamii ambayo ni maarufu kwa majigambo.Huu ni utafiti wa kitaaluma uliofanywa na Rubanza (2004) na Method Samwel ,hawa wote wameangalia jamii ya wahaya.
Katika jamii ya wahaya majigambo yalikuwa na muktadha wake maalum walikuwa wanatamba mbele ya mtemi kabla ya kwenda vitani au baada ya kurudi toka vitani n.k
Ø Kwa wahaya mjigambi hujigamba mbele ya watu ,sherehe ambayo inahudhuriwa na mtemi na kuna namna ya kuanza na kumaliza.Mfano wakati wa kuanza mjigambi anaweza kuanza kwa kujitambulisha kwa kujigamba na anaweza kumalizia kwa shukrani au heshima kwa mtemi au kiongozi aliyepo pale.
Ø Katika majigambo ,mjigambi yupo huru kutumia lugha ya kujikweza akiwa amevaa maleba maalumu mfano katika kujigamba mjigambi anavaa kanzu ndefu au nguo za majani ya migomba na hushika silaha kama vile mkuki ,panga,n.k
Ø Pia majigambo huambatana na ngoma yenye mapigo ya pekee na maandamano fulani.
Ø Katika majigambo kuna zawadi,shujaa aliyeshinda au aliyerudi toka kuwinda ,vitani n.k hupewa zawadi kama pombe.
Ø Wale walioenda vitani au kuwinda wakashindwa zawadi yao ilikuwa maji ya kunywa na kinyesi cha ng’ombe.Hii ilikuwa inaleta umakini kwani kurudi na kinyesi ilikuwa ni aibu.
Miaka ya 1960 utendaji katika majigambo uliathiriwa sana kutokana na mabadiliko ya kijamii na kiutawala
Sunday, 23 September 2018
FASIHI
Imetayarishwa na
Mwl.Albert J.Safari
Simu:0715803005
Barua pepe:salbertode@yahoo.com
Fasihi (kutoka neno la Kiarabu ﻓﺼﺎﺣﺔ
fasaha kwa maana ulumbi) ni utanzu (tawi ) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe kwa
hadhira husika. Ni ufundi wa kuwasilisha mawazo au ujumbe ulio katika fikra za binadamu .
Vipengele vinavyounda fani ya fasihi ni kama ifuatavyo: fani ni umbo la nje la
kazi ya fasihi; maudhui ni umbo lake la ndani.
Fani
Katika kazi yoyote ya fasihi ni lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji au wasomaji) husika. Ustadi (ufundi) huo unaovutia hadhira huitwa fani, ambayo hujumuisha mambo kama vile:
Muundo - ni mtitiriko/msuko/mpangilio wa matukio / visa
Mtindo - ni mbinu inayotumiwa na fanani ili atofautiane na fanani mwingine
Wahusika - ni watu au vitu vyenye
uhai au la ambavyo hutumiwa na fanani katika kazi yake
Mandhari - ni eneo ambalo fanani hulitumia kujenga matukio na au mtiriko katika kuumba kazi yake
Matumizi ya lugha - ni lugha anayotumia fanani katika kujenga wasifu wa wahusika kihaiba kazi yake
Maudhui
Pamoja na fani, kazi yoyote ya fasihi huwa na ujumbe na malengo mbalimbali ambayo hukusudiwa yaifikie jamii husika. Yale yote ambayo msanii wa kazi ya fasihi anakusudia yaifikie jamii husika huitwa maudhui. Maudhui ya kazi ya fasihi hujumuisha:
Dhamira
Ujumbe/Mafunzo
Mgogoro
Falsafa/msimamo na
Mtazamo
Sifa za fasihi
Fasihi ni utanzu wa sanaa. Kuna aina tatu za sanaa: sanaa za ghibu, sanaa za maonyesho na sanaa za vitendo.
Kazi ya fasihi ni kujaribu kusawiri vipengele vya maisha, mahusiano, na hisia za watu katika jamii husika.
Fasihi ni maelezo ya fani na maudhui.
Fasihi ni ufundi unaotumia lugha ili kulete mguso au hisia fulani za watu katika muktadha fulani.
Dhima za fasihi katika maisha
Fasihi hufanya kazi mbalimbali katika maisha:
Kuelimisha jamii-Fasihi hutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii wanaweza kuelimishwa juu ya mambo mabalimbali, kama vile juu ya umuhimu wa kuishi kwa amani, umuhimu wa kijikomboa kifikra, umuhimu wa kujikomboa kiuchumi, ubaya wa ufisadi na kadhalika.
Kukuza utamaduni -Kupitia fasihi simulizi, tamaduni na mila za jamii husika huhifadhiwa. Kwa mfano kupitia methali, misemo, nahau na vitendawili unaweza kujua mila na tamaduni za jamii husika.
Kukuza lugha-Fasihi hutumia lugha kufikisha ujumbe wake katika jamii, lugha ya fasihi huwa ni ya kisanaa zaidi na hivyo kuifanya iwe yenye mvuto kwa wasikilizaji au wasomaji. Mtu anaposoma au kusikiliza kazi ya fasihi anapata ujuzi wa lugha. Lakini pia fasihi yenyewe inaweza kutumika kama chombo cha kukuza lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na utajiri mkubwa wa lugha.
Kuburudisha jamii-Pamoja na mambo mengine fasihi inalenga kuburudisha jamii. Kupitia takribani vipera vyake vyote, fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira, kwa mfano kupitia nyimbo, hadithi, mashairi na kadhalika.
Kukomboa jamii.
Kuonya jamii-Fasihi ina jukumu la kuhakikisha wanajamii wanakaa katika mstari wa maadili ya jamii husika. Kupitia fasihi wanajamii wanapewa mwongozo wa jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.
Kukuza uwezo wa kufikiri-Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. Kwa mfano, vitendawili, ngano za mtanziko na kadhalika.
Aina za fasihi
Fasihi ndiyo aina pekee ya sanaa inayotumia lugha kujitambulisha au kujitofautisha na aina nyingine za sanaa. Kuna aina kuu mbili za fasihi nazo ni:
Fasihi simulizi - huwasilishwa kwa lugha ya mazungumzo/masumilizi
Fasihi andishi - huwasilishwa kwa lugha ya maandishi
Fasihi hizi zina dhima sawa katika jamii ingawa ni tofauti. Utofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi hujitokeza katika uwasilishwa wake katika jamii husika.
Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya mazungumzo au masimulizi ya mdomo
Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya maandishi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mazungumzo ya mdomo ili kufikisha ujumbe kwa hadhira. Aina hii ya fasihi ndiyo iliyokuwapo tangu zamani kabisa mwanadamu alipoanza kuishi yaani ilianza pale mwanadamu alipochangamana na wenzake katika kufanya mambo mbalimbali mfano,shughuli za biashara,kilimo,na nyinginezo.
Utanzu huu wa fasihi simulizi una vipera au aina kuu nne, nazo ni:
1. Hadithi.
2. Ushairi.
3. Semi.
4. Maigizo.
Sifa za fasihi simulizi
Hutolewa kwa njia ya mdomo.
Haitumii gharama
Huonyesha uhalisia wa hisia za mzungumzaji
Ni mali ya jamii. Hakuna mtu anayeimiliki.
Dhima za fasihi simulizi
kuburudisha
kuelimisha jamii
kunasihi
kukuza lugha
kuunganisha watu
Kufanana kwa fasihi simulizi na fasihi andishi
Kimsingi fasihi ni moja ingawa imegawanyika katika sehemu kuu mbili, yaani, fasihi simulizi na fasihi andishi. Mbali na mgawanyiko huo kuna mambo ambayo yanafanana katika fasihi zote mbili. Mambo hayo ni pamoja na:
Zote hutumia ufundi wa lugha ili kuwasilisha ujumbe kwa hadhira husika
Zote zina dhima inayofanana katika jamii, yaani, kuelimisha na kuburudisha jamii
Zote zina wahusika ambao ni Fanani na Hadhira
Zote zina vipengele vya Fani na Maudhui
zote zinaweza kukashifiwa na wasanii mbalimbali ikiwa hawajaridhishwa na mbinu za lugha zilizotumika
Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi
Na. Kipengele Fasihi simulizi Fasihi andishi
1 Uwasilishwaji
Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo pamoja na vitendo
Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi bila vitendo
2 Umri
Fasihi simulizi ni kongwe kuliko fasihi andishi
Fasihi andishi ni changa kuliko fasihi simulizi
3 Umilikaji
Fasihi simulizi humilikiwa na jamii nzima, ni mali ya jamii
Fasihi andishi humilikiwa na mwandishi, ni mali ya mwandishi
4 Tanzu
Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi
Fasihi andishi ina tanzu chache kuliko fasihi simulizi
5 Hadhira
Hadhira ya fasihi simulizi ni watu wote katika jamii
Hadhira ya fasihi andishi ni wale tu wanaojua kusoma na kuandika
6 Mabadiliko
Fasihi simulizi hubadilika haraka kutegemeana na mahitaji ya hadhira na wakati
Fasihi andishi haibadiliki haraka kutegemeana na mahitaji ya hadhira na wakati
7 Utunzi
Fasihi simulizi hutungwa kwa muda mfupi
Fasihi andishi hutungwa kwa muda mrefu
8
Mazingira ya uwasilishaji wake (mandhari)
Huambatana na tukio maalumu la jamii
Kusoma au kusomewa ni ya kufikirika au mahali popote
9 Marekebisho
Mtunzi/msimulizi anaweza kurekebisha kazi yake wakati wa kuwasilisha au baadaye kidogo
Kitabu kikishaandikwa ni vigumu kukifanyia marekebisho mpaka toleo jipya litakapoandikwa
10 Uhifadhi
Huhidhiwa kwa njia ya kichwa (kichwani) kwa sehemu kubwa na sehemu ndogo sana huhifadhiwa kwenye maandishi, vinasa sauti au kanda mbalimbali za kurekodi
Huhifadhiwa kwa njia ya maandishi (vitabu)
11 Gharama
Fasihi andishi ina gharama ndogo ukilinganisha na fasihi andishi
Fasihi andishi ina gharama kubwa ukilinganisha na fasihi simulizi
12 Wahusika
Fasihi simulizi mara nyingi hutumia wahusika wa kubuni wasio binadamu
Fasihi andishi hutumia wahusika wa kubuni ambao mara nyingi ni binadamu
13 Uhai
Fasihi simulizi ni hai kuliko fasihi andishi
Fasihi andishi si hai kuliko fasihi simulizi

FASIHI ANDISHI
Fasihi andishi ni sanaa itumiayo
maandishi kufikisha ujumbe kwa
hadhira iliyokusudiwa
Fasihi andishi hugawanyika katika matawi mawili: nathari na ushairi .
Pia fasihi andishi ina tanzu nyingi mbalimbali, hasa hadithi fupi, riwaya ,
tamthiliya , insha, shairi n.k.
Kulingana na mada ya kazi ya kifasihi, inawezekana kutofautisha bunilizi na kazi zinazowakilisha ukweli .
Sifa za fasihi andishi
Ni mali ya mtu binafsi
Hupitishwa kwa njia ya maandishi
Haiwezi kubadilishwa papo kwa papo
Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa katika uwasilishaji wake
Huweza kutunzwa kwa muda mrefu.
Dhima za fasihi andishi
Kukuza lugha
Kuburudisha
Kuelimisha
Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi.
FASIHI SIMULIZI
Imetayarishwa na,
Mwl.Albert J. Safari
Simu: 0715803005
Barua pepe:salbertode@yahoo.com
Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti na
maandishi kama kwenye fasihi andishi ) kama njia kuu maalum ya kufikisha
ujumbe . Ni sehemu ya msingi ya
utamaduni , na vipengele vyake vingi vinafanya kazi kama katika fasihi kwa jumla.
Katika jamii isiyo na uandishi ni wazi kuwa hakuna fasihi andishi. Hata hivyo kila jamii ina hazina ya mapokeo yapokelewayo mdomo kwa mdomo—kwa mfano utenzi, ngano au nyimbo za jadi —hivyo vyote ni sehemu za fasihi simulizi.
Hata jamii ijuayo kusoma na kuandika inaendelea kuwa na fasihi simulizi, hasa nyumbani , k.m. katika kuwasimulia watoto hadithi. Lakini mara nyingi fasihi simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika, na mitindo ya masimulizi yake haiendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi.
Sifa za fasihi simulizi
Fasihi simulizi ina sifa za pekee ambazo huipambanua na fasihi andishi. Sifa hizo ndizo huipa uhai fasihi hii. Miongoni mwa sifa hizo ni pamoja na:
1. Utendaji wa fasihi simulizi hushirikisha utendaji wa fanani na hadhira moja kwa moja (ana-kwa-ana)
2. Fanani kuwepo kwa fanani ambaye husimulia, huimba, hupiga makofi na hata kubadilisha miondoko na mitindo ya usimuliaji.
3. Hadhira kuwepo kwa hadhira ambayo hushiriki kwa kuuliza maswali, kupiga makofi, kushangilia, kuimba na kadhalika - kutegemeana na jinsi ambavyo fanani atawashirikisha.
4. Fasihi simulizi huendana na wakati na mazingira; baadhi ya tanzu au vipera vya fasihi simulizi vinaweza kuwa vimepitwa na wakati, lakini bado vinaweza kubadilishwa na vikasadifu wakati mahususi.
5. Fasihi simulizi ni mali ya jamii nzima , humilikiwa na kila mtu katika jamii. Sifa hii ndiyo huipa uwezo wa kurithishwa toka kizazi kimoja kwenda kingine.
6. Fasihi simulizi huzaliwa, hukua na hata kufa . Kuzaliwa: fasihi simulizi huzaliwa kutokana na mambo yanayotokea katika jamii. Kukua: fasihi simulizi hukua kadIri inavyojadili matatizo yanayojitokeza. Kufa: fasihi simulizi hufa kwa namna mbili. Hii ni kutokana na maendeleo ya mazingira ambayo hufuata mfumo wa jamii husika. Kwa mfano kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia fasihi inaweza kuhifadhiwa kwenye
maandishi na kwenye kanda mbalimbali za kurekodi.
7. Fasihi simulizi ina uwanja maalumu wa kutendea; ni sehemu ambayo imetengwa rasmi kwa ajili ya aina/kipera fulani cha fasihi simulizi. Sehemu hiyo inaweza kuwa porini, misituni, mtoni, pangoni, nyumbani na kadhalika.
8. Fasihi simulizi ina sifa ya "kuwa na utegemezi".Utegemezi wa fasihi simulizi hutegemea zaidi sanaa za maonesho hasa sanaa za ghibu yaani muziki,kwa sababu,fasihi simulizi huchota uhai wake kutokana na vitendo na tabia za fanani,mahadhi na toni za kimuziki na vipengele vingine vya sanaa za maonesho.
Tanzu na vipera vya fasihi simulizi
Hadithi Ushairi Semi sanaa za maonesho
Ngano Mashairi Methali Matambiko
Vigano Tenzi Nahau Majigambo
Soga Tendi Misemo Mivigha
Visakale Ngonjera Mafumbo Utani
Visasili Nyimbo Vitendawili Vichekesho
Hekaya Maghani Mizungu Ngoma
Arafa Michezo ya jukwaani
Michezo ya watoto
Ngonjera
Maigizo
Hadithi
Masimulizi ni fasihi yenye kusimulia habari fulani. Ni masimulizi ambayo yanatumia lugha ya mjazo au nathari na mtiririko wake huwa mwepesi au sahili. Urefu wa hadithi hutofautiana kutoka kitanzu/kipera kimoja hadi kingine. Kwa jumla zipo hadithi ambazo ni za kubuni na zingine za kihistoria.
Baadhi ya vipera vya utanzu huu ni:
Ngano
Hizi ni hadithi za kimapokeo zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu katika kuelezea au kuonya kuhusu maisha. Vijipera vya kipera hiki ni:
Soga
Ni hadithi ndogo ndogo zinazohusisha utani na ucheshi kwa kiasi fulani. Hizi ni hadithi ambazo hutambwa katika mtiririko wa matukio ambao huzua kicheko. Soga hudhamiria kuchekesha na pia kukejeli.
Visakale
Masimulizi ya kimapokeo juu ya wahenga au mashujaa wa kabila au taifa yenye kuchanganya chuku na historia. Kwa mfano hadithi za Liyongo.
Mapisi
Maelezo ya historia bila kutia mambo ya kubuni.
Tarihi
Hizi ni hadithi ambazo husimulia au zimejengwa kwenye matukio ya kihistoria. Inawezekana matukio yanayosimuliwa yakawa ya kweli, yaani yalipata kutokea kihistoria. Hadithi hizi hutokea zaidi katika maandishi.
Visasili
Ni utanzu unaofungamana na imani za dini na mizungu ya jamii. Hizi ni hadithi za kale zenye kuwakilisha imani na mtazamo wa jamii inayohusika kuhusu asili ya ulimwengu na mwenendo wake, kuhusu asili yao wenyewe, na maana na shabaha ya maisha yao. Mara nyingi hadithi hizi huaminiwa kuwa ni kweli tupu, na hutumika kuelezea au kuhalalisha baadhi ya mila na madhehebu ya jamii inayohusika.
Ushairi
Huu ni utanzu wa fasihi simulizi unaowasilishwa kwa hadhira kwa njia ya uimbaji au ughani badala ya usemaji wa kawaida. Katika utanzu huu kuna vipera viwili ambavyo ni nyimbo na maghani.
Nyimbo
Nyimbo ni kila kinachoimbwa. Kipera hiki kimegawanyika katika vijipera vifuatavyo ambavyo ni, tumbuizo, bembea, kongozi, nyimbo za dini, wawe, tenzi, tendi, mbolezi, kimai, nyiso, nyimbo za vita, nyimbo za uwindaji, nyimbo za taifa.
Maghani
Maghani ni istilahi inayotumiwa kuelezea aina ya ushairi ambao hutolewa kwa kalima au maneno badala ya kuimbwa. Kipera hiki kina vijipera vitatu ambavyo ni maghani ya kawaida, sifo na maghani masimulizi.
Maghani ya kawaida
Hilo ni kundi ambalo tunaweza kuingiza fani mbalimbali za ushahiri simulizi kama vile ushairi wa mapenzi, siasa, maombolezo, kazi, dini ilimradi unaghanwa katika namna ya uwasilishwaji wake.
Sifo
Hizi ni tungo za kusifu ambazo husifu watu, wanyama na mimea. Baadhi ya sifo huwa zinakashifu au kukejeli. Sifo huwa na tanzu muhimu kama vile vivugo (majigambo), pembezi na tondozi.
Semi
Semi ni tungo au kauli fupifupi za kisanaa zitumiazo picha na tamathali kuelezea maudhui yanayobeba maana au mafunzo muhimu kwa jamii. Kundi hili lina vipera au tanzu sita ambazo ni:
Methali
Vitendawili
Nahau
Misemo
Mafumbo
Mizungu
Lakabu
Methali
Methali ni semi fupi fupi zenye mpangilio maalumu wa maneno ambazo huelezea kwa muhtasari mafunzo, mafumbo na mawazo mazito yaliyotokana na uzoefu wa kijamii. Mara nyingi mawazo hayo huelezwa kwa kutumia tamathali hasa sitiari na mafumbo.
Methali nyingi huundwa na vipande viwili vya maneno vyenye fikra yurani. Kipande cha kwanza huashiria tendo au sharti na kipande cha pili huashiria matokeo ya tendo au sharti hilo. Au sehemu ya kwanza huanzisha wazo fulani, na sehemu ya pili hulikanusha au kulikamilisha wazo hilo. Kwa mfano; mwenda pole hajikwai, aliye juu mngoje chini.
Mifano ya methali
Mcheka kilema,hali hakija mfika.
Kupotea njia, ndiko kujua njia.
Mchelea mwana kulia, utalia wewe.
Maana ya methali hutegemea muktadha au wakati maalumu katika jamii.
Kazi za methali
Methali zina kazi nyingi katika jamii yoyote ile kama vile:
Kuionya jamii inayohusika au inayopewa methali hiyo.
Kuishauri jamii inayopewa au kutamkiwa methali hiyo.
Kuihiza jamii inayohusika.
Kukejeli mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya jamii husika.
Vitendawili
Ni semi zilizofumbwa ambazo hutolewa kwa hadhira ili izifumbue. Fumbo hilo kwa kawaida huwa linafahamika katika jamii hiyo, na mara nyingi lina mafunzo muhimu kwa washiriki, mbali na kuwachemsha bongo zao. Vitendawili ni sanaa inayotegemea uwezo wa mtu kutambua, kuhusisha na kulinganisha vitu vya aina mbalimbali vilivyomo katika maumbile.
Misimu
Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Msimu ukipata mashiko ya kutosha katika jamii huweza hatimaye kuingia katika kundi la methali za jamii hiyo.
Mafumbo
Ni semi za maonyo au mawaidha ambazo maana zake za ndani zimefichika. Fumbo hubuniwa na msemaji kwa shabaha na hadhira maalum, hivyo ni tofauti na methali au vitendawili ambavyo ni semi za kimapokeo.
Lakabu
Haya ni majina ya kupanga ambayo baadhi ya watu hupewa au hujipatia kutokana na sifa zao za kimwili, kinasaba, kitabia au kimatendo. Majina haya huwa ni maneno au mafungu ya maneno yenye maana iliyofumbwa. Mara nyingi majina haya huwa ni sitiari. Baadhi ya majina haya humsifia mhusika, lakini mengine humkosoa au hata kumdhalilisha; Mifano: simba wa yuda- Hali Selassie, Baba wa taifa – Mwl Nyerere.
Sanaa za maonesho.
Ni maonesho au maigizo ambayo hutumia watendaji na mazingira maalumu kwa kuiga tabia na matendo ya watu au viumbe wengine ili kuburudisha na kutoa ujumbe fulani kwa hadhira.

Subscribe to:
Posts (Atom)
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU) BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...
-
VERB TENSES Prepared By:Sir.Albert J.Safar Mobile NO. +255 715 803 005 Mail Address: salbertode@yahoo.com Verbs come in t...
-
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU) BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...
-
HISTORY NOTES FOR FORM FOUR & FORM THREE New Syllabus 2010 Prepared By: Sir. Alberto De Safari Mail Address: salbe...