SUALA LA UTENDAJI KATIKA FASIHI SMULIZI
Katika fasihi simulizi utendaji ni uti wa mgongo yaani ni suala la msingi.
Mulokozi (1996:24) Fasihi simulizi ni tukio na linafungamana na matukio ya kijamii na hutawaliwa na fanani (msanii au mtendaji)
Ø Fanani ni mtendaji au mwasilishaji na mtunzi wa kipera,fani husika kwa hadhira katika muktadha wa tukio fulani ,kazi yake yaweza kuwa kichwani au akatunga papo kwa papo.
Ø Fani inayotendwa au kipera
Ø Hadhira/wasikilizaji,washiriki,wachangiaji ,wahakiki,watazamaji hawa huangalia uzuri au ubaya.
Ø Tukio-ni shughuli yoyote ya kijamii ambayo ndio muktadha wa utendaji.mfano msiba,ibada,harusi,sherehe,n.k
Ø Mahali –eneo mahsusi ambapo sanaa hiyo inatendwa.
Ø Wakati na muda maalum au majira maalum ya utendaji .Vipera vingi vina wakati wake.mfano Sifo huimbwa wakati wa kuomba.Mwingiliano huu wa vipengele hivi ndiyo unaoamua fani hiyo iwasilishwe vipi.
OKPEWHO (1992) Anasema Utendaji unaotofauta kutokana na sababu mbali mbali kama vile;
Ø Umri wa fanani
Ø Umri wa hadhira
Ø Nguvu ya fanani,baadhi ya vipera vinahitaji fanani awe na nguvu mfno majigambo
Ø Tukio husika mfano Msiba hauwezi kufanana na sherehe
Ø Aina ya mandhari au jukwaa maalum la kutendea yaani pale inapotendewa.
Ø Vifaa ambatani vinavyotumika na fanani katika utendaji mfano maleba,mkuki
Ø Idadi ya fanani
Pia utendaji unatokana au unatawaliwa na;
Ø Dhima ya kipera( tukio ),muktadha wa uwasilishaji na namna ya uwasilishaji hutegemea dhima ya kipera katika jamii.
Ø Muda na mahali,ni muhimu kuzingatia kwa kipera chochote hutegemea au husukumwa na muda na mahali.mfano matambiko yanafanywa muda gani?
Ø Mila na utamaduni ,kila jamii ina mila na utamaduni wake na hivyo huathiri utendaji wa vipera husika.mfano Mavazi au maleba maalum ya kisanaa yaani kipera hiki kinahitaji aina ipi ya maleba?
Ø Sifa za wahusika au watendaji wa kipera fulani wanapaswa wawe akina nani?
SWALI; JE UTENDAJI NI NINI?
Muluka (1999) anasema Utendaji ni uwasilishaji wa hadithi au ngano unaofanywa na msanii kwa hadhira kwa kutumia mdomo na kuambatana na matendo ya viungo mbalimbali vya mwili na ishara uso.Hivyo kila kipera kipo kwaajili ya kutendwa.
UTENDAJI KATIKA VIPERA MBALI MBALI
Finnegan (1970) ‘’ Oral Literature in Africa’’ anasema kuwa katika utendaji kuna kanuni maalum,jamii nyingi zina utamaduni wake.Hadithi ni utanzu muhimu katika jamii za kiafrika.Hadithi ni utanzu wa jioni na mtambaji anazungukwa na hadhira.
SWALI; Je kwanini hadithi inatambwa jioni?
Ø K wasababu mchana mtambaji anakuwa katika utafutaji yaani katika shughuli zake za kila siku.
Ø Hadithi ina fomula zake za kuanza na kumalizia yaani mianzo na miisho maalum ya kihadithi.
Ø Katika kutamba hadithi fanani habanwi kutumia vipera vingine katika utendaji wake.
Ø Katika kutamba hadithi msimuliaji hatakiwi kukalili ila anapaswa kuleta upya fulani wa utendaji wa hadithi hiyo.
Ø Mtambaji anapaswa kutumia sauti vizuri na iendane na utanzu wenyewe.
Ø Kuna wasimuliaji wazuri na wabaya au wasiowazuri
Ø Msimuliaji awe mbunifu ili kunogesha hadithi
Ø Katika utendaji msimuliaji aoneshe hisia zake.
UFALAGUZI
Ni uwezo alionao fanani katika kuunda kutunga ,kugeuza na kuiwasilisha kazi ya fasihi simulizi papo kwa papo bila ya kujifunga na muundo asilia au na muundo uliozoeleka. Hivyo katika utendaji wa kipera fulani kuna utungaji mpya kutokana na mbinu fulani unazotumia.
Ø Hivyo hadithi moja inaweza simuliwa tofauti na wasimuliaji tofauti.Utendaji wa kipera hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine.
SIFA ZA FANANI BORA
Senkoro anasema Fanani bora anatakiwa afanye kazi ya ualimu ,awe mtoa maoni,msanii,mburudishaji,muigizaji
Ø Fanani aifanye hadithi ionekane mpya kila mara anaposimulia.
Ø Fanani aifurahie na kujivunia fani anayoitenda,kuisimulia ipasavyo.
Ø Fanani awe mbunifu na awe na kumbukumbu.
Ø Suala la utamaduni katika utendaji fanani azingatie utamaduni wa kipera anachotamba.
Ø Fanani awe tajiri wa lugha yaani ajue kutumia mbinu mbalimbali za lugha kama vile nahau,semi,n.k.
Ø Fanani asiwe na aibu katika utendaji atumie vema lugha na viungo mbali mbali.
Ø Kujua mambo ya kihistoria kwani Fasihi inapitia vipindi mbalimbali.
UTENDAJI WA KIPERA CHA SEMI
1. METHALI
Ni usemi mfupi wa kimapokeo unaodokeza mafumbo mazito au fikra zinazotokana na uzoefu wa jamii husika.Katika utendaji unaweza kutofautiana na vipera vingine kwani utendaji wa methali lazima unajitegemeza wakati wa kutenda fani nyingine mfano mkutano,maongezi ya kawaida,majadiliano,hadithi,wakati wa kukanya mtu n.k.
Kimsingi watambaji wa methali ni watu wazima (wazee) kutokana na kuishi kwao katika jamii kwa muda mrefu.
2. VITENDAWILI
Utendaji katika vitendawili si tegemezi kama methali bali kitendawili kinasimama chenyewe kwa kufuata kanuni zilizowekwa na jamii husika.Mfano katika kabila la wajaluo ukishindwa kutegua unaombwa mke au mme na katika jamii nyingine unapewa mji.
2. MAJIGAMBO
Katika Jamii ya wahaya ni jamii ambayo ni maarufu kwa majigambo.Huu ni utafiti wa kitaaluma uliofanywa na Rubanza (2004) na Method Samwel ,hawa wote wameangalia jamii ya wahaya.
Katika jamii ya wahaya majigambo yalikuwa na muktadha wake maalum walikuwa wanatamba mbele ya mtemi kabla ya kwenda vitani au baada ya kurudi toka vitani n.k
Ø Kwa wahaya mjigambi hujigamba mbele ya watu ,sherehe ambayo inahudhuriwa na mtemi na kuna namna ya kuanza na kumaliza.Mfano wakati wa kuanza mjigambi anaweza kuanza kwa kujitambulisha kwa kujigamba na anaweza kumalizia kwa shukrani au heshima kwa mtemi au kiongozi aliyepo pale.
Ø Katika majigambo ,mjigambi yupo huru kutumia lugha ya kujikweza akiwa amevaa maleba maalumu mfano katika kujigamba mjigambi anavaa kanzu ndefu au nguo za majani ya migomba na hushika silaha kama vile mkuki ,panga,n.k
Ø Pia majigambo huambatana na ngoma yenye mapigo ya pekee na maandamano fulani.
Ø Katika majigambo kuna zawadi,shujaa aliyeshinda au aliyerudi toka kuwinda ,vitani n.k hupewa zawadi kama pombe.
Ø Wale walioenda vitani au kuwinda wakashindwa zawadi yao ilikuwa maji ya kunywa na kinyesi cha ng’ombe.Hii ilikuwa inaleta umakini kwani kurudi na kinyesi ilikuwa ni aibu.
Miaka ya 1960 utendaji katika majigambo uliathiriwa sana kutokana na mabadiliko ya kijamii na kiutawala
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU) BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...
-
VERB TENSES Prepared By:Sir.Albert J.Safar Mobile NO. +255 715 803 005 Mail Address: salbertode@yahoo.com Verbs come in t...
-
HISTORY NOTES FOR FORM FOUR & FORM THREE New Syllabus 2010 Prepared By: Sir. Alberto De Safari Mail Address: salbe...
-
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU) BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...
Ni kazi nzuri. Muwe mnaweka marejeleo ya kazi yenu.
ReplyDeleteKweli kabisa au mmefanya udukuzi mazee!!!?
DeleteKazi nzuri.heko!!!
ReplyDeleteMkifanya kazi kama hizi msisahau marejeleo
ReplyDeleteMkifanya kazi kama hizi msisahau marejeleo
ReplyDelete