Imetayarishwa na
Mwl.Albert J.Safari
Simu:0715803005
Barua pepe:salbertode@yahoo.com
Fasihi (kutoka neno la Kiarabu ﻓﺼﺎﺣﺔ
fasaha kwa maana ulumbi) ni utanzu (tawi ) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe kwa
hadhira husika. Ni ufundi wa kuwasilisha mawazo au ujumbe ulio katika fikra za binadamu .
Vipengele vinavyounda fani ya fasihi ni kama ifuatavyo: fani ni umbo la nje la
kazi ya fasihi; maudhui ni umbo lake la ndani.
Fani
Katika kazi yoyote ya fasihi ni lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji au wasomaji) husika. Ustadi (ufundi) huo unaovutia hadhira huitwa fani, ambayo hujumuisha mambo kama vile:
Muundo - ni mtitiriko/msuko/mpangilio wa matukio / visa
Mtindo - ni mbinu inayotumiwa na fanani ili atofautiane na fanani mwingine
Wahusika - ni watu au vitu vyenye
uhai au la ambavyo hutumiwa na fanani katika kazi yake
Mandhari - ni eneo ambalo fanani hulitumia kujenga matukio na au mtiriko katika kuumba kazi yake
Matumizi ya lugha - ni lugha anayotumia fanani katika kujenga wasifu wa wahusika kihaiba kazi yake
Maudhui
Pamoja na fani, kazi yoyote ya fasihi huwa na ujumbe na malengo mbalimbali ambayo hukusudiwa yaifikie jamii husika. Yale yote ambayo msanii wa kazi ya fasihi anakusudia yaifikie jamii husika huitwa maudhui. Maudhui ya kazi ya fasihi hujumuisha:
Dhamira
Ujumbe/Mafunzo
Mgogoro
Falsafa/msimamo na
Mtazamo
Sifa za fasihi
Fasihi ni utanzu wa sanaa. Kuna aina tatu za sanaa: sanaa za ghibu, sanaa za maonyesho na sanaa za vitendo.
Kazi ya fasihi ni kujaribu kusawiri vipengele vya maisha, mahusiano, na hisia za watu katika jamii husika.
Fasihi ni maelezo ya fani na maudhui.
Fasihi ni ufundi unaotumia lugha ili kulete mguso au hisia fulani za watu katika muktadha fulani.
Dhima za fasihi katika maisha
Fasihi hufanya kazi mbalimbali katika maisha:
Kuelimisha jamii-Fasihi hutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii wanaweza kuelimishwa juu ya mambo mabalimbali, kama vile juu ya umuhimu wa kuishi kwa amani, umuhimu wa kijikomboa kifikra, umuhimu wa kujikomboa kiuchumi, ubaya wa ufisadi na kadhalika.
Kukuza utamaduni -Kupitia fasihi simulizi, tamaduni na mila za jamii husika huhifadhiwa. Kwa mfano kupitia methali, misemo, nahau na vitendawili unaweza kujua mila na tamaduni za jamii husika.
Kukuza lugha-Fasihi hutumia lugha kufikisha ujumbe wake katika jamii, lugha ya fasihi huwa ni ya kisanaa zaidi na hivyo kuifanya iwe yenye mvuto kwa wasikilizaji au wasomaji. Mtu anaposoma au kusikiliza kazi ya fasihi anapata ujuzi wa lugha. Lakini pia fasihi yenyewe inaweza kutumika kama chombo cha kukuza lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na utajiri mkubwa wa lugha.
Kuburudisha jamii-Pamoja na mambo mengine fasihi inalenga kuburudisha jamii. Kupitia takribani vipera vyake vyote, fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira, kwa mfano kupitia nyimbo, hadithi, mashairi na kadhalika.
Kukomboa jamii.
Kuonya jamii-Fasihi ina jukumu la kuhakikisha wanajamii wanakaa katika mstari wa maadili ya jamii husika. Kupitia fasihi wanajamii wanapewa mwongozo wa jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.
Kukuza uwezo wa kufikiri-Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. Kwa mfano, vitendawili, ngano za mtanziko na kadhalika.
Aina za fasihi
Fasihi ndiyo aina pekee ya sanaa inayotumia lugha kujitambulisha au kujitofautisha na aina nyingine za sanaa. Kuna aina kuu mbili za fasihi nazo ni:
Fasihi simulizi - huwasilishwa kwa lugha ya mazungumzo/masumilizi
Fasihi andishi - huwasilishwa kwa lugha ya maandishi
Fasihi hizi zina dhima sawa katika jamii ingawa ni tofauti. Utofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi hujitokeza katika uwasilishwa wake katika jamii husika.
Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya mazungumzo au masimulizi ya mdomo
Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya maandishi
Fasihi simulizi
Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mazungumzo ya mdomo ili kufikisha ujumbe kwa hadhira. Aina hii ya fasihi ndiyo iliyokuwapo tangu zamani kabisa mwanadamu alipoanza kuishi yaani ilianza pale mwanadamu alipochangamana na wenzake katika kufanya mambo mbalimbali mfano,shughuli za biashara,kilimo,na nyinginezo.
Utanzu huu wa fasihi simulizi una vipera au aina kuu nne, nazo ni:
1. Hadithi.
2. Ushairi.
3. Semi.
4. Maigizo.
Sifa za fasihi simulizi
Hutolewa kwa njia ya mdomo.
Haitumii gharama
Huonyesha uhalisia wa hisia za mzungumzaji
Ni mali ya jamii. Hakuna mtu anayeimiliki.
Dhima za fasihi simulizi
kuburudisha
kuelimisha jamii
kunasihi
kukuza lugha
kuunganisha watu
Kufanana kwa fasihi simulizi na fasihi andishi
Kimsingi fasihi ni moja ingawa imegawanyika katika sehemu kuu mbili, yaani, fasihi simulizi na fasihi andishi. Mbali na mgawanyiko huo kuna mambo ambayo yanafanana katika fasihi zote mbili. Mambo hayo ni pamoja na:
Zote hutumia ufundi wa lugha ili kuwasilisha ujumbe kwa hadhira husika
Zote zina dhima inayofanana katika jamii, yaani, kuelimisha na kuburudisha jamii
Zote zina wahusika ambao ni Fanani na Hadhira
Zote zina vipengele vya Fani na Maudhui
zote zinaweza kukashifiwa na wasanii mbalimbali ikiwa hawajaridhishwa na mbinu za lugha zilizotumika
Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi
Na. Kipengele Fasihi simulizi Fasihi andishi
1 Uwasilishwaji
Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo pamoja na vitendo
Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi bila vitendo
2 Umri
Fasihi simulizi ni kongwe kuliko fasihi andishi
Fasihi andishi ni changa kuliko fasihi simulizi
3 Umilikaji
Fasihi simulizi humilikiwa na jamii nzima, ni mali ya jamii
Fasihi andishi humilikiwa na mwandishi, ni mali ya mwandishi
4 Tanzu
Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi
Fasihi andishi ina tanzu chache kuliko fasihi simulizi
5 Hadhira
Hadhira ya fasihi simulizi ni watu wote katika jamii
Hadhira ya fasihi andishi ni wale tu wanaojua kusoma na kuandika
6 Mabadiliko
Fasihi simulizi hubadilika haraka kutegemeana na mahitaji ya hadhira na wakati
Fasihi andishi haibadiliki haraka kutegemeana na mahitaji ya hadhira na wakati
7 Utunzi
Fasihi simulizi hutungwa kwa muda mfupi
Fasihi andishi hutungwa kwa muda mrefu
8
Mazingira ya uwasilishaji wake (mandhari)
Huambatana na tukio maalumu la jamii
Kusoma au kusomewa ni ya kufikirika au mahali popote
9 Marekebisho
Mtunzi/msimulizi anaweza kurekebisha kazi yake wakati wa kuwasilisha au baadaye kidogo
Kitabu kikishaandikwa ni vigumu kukifanyia marekebisho mpaka toleo jipya litakapoandikwa
10 Uhifadhi
Huhidhiwa kwa njia ya kichwa (kichwani) kwa sehemu kubwa na sehemu ndogo sana huhifadhiwa kwenye maandishi, vinasa sauti au kanda mbalimbali za kurekodi
Huhifadhiwa kwa njia ya maandishi (vitabu)
11 Gharama
Fasihi andishi ina gharama ndogo ukilinganisha na fasihi andishi
Fasihi andishi ina gharama kubwa ukilinganisha na fasihi simulizi
12 Wahusika
Fasihi simulizi mara nyingi hutumia wahusika wa kubuni wasio binadamu
Fasihi andishi hutumia wahusika wa kubuni ambao mara nyingi ni binadamu
13 Uhai
Fasihi simulizi ni hai kuliko fasihi andishi
Fasihi andishi si hai kuliko fasihi simulizi
Sunday, 23 September 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU)
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU) BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...
-
VERB TENSES Prepared By:Sir.Albert J.Safar Mobile NO. +255 715 803 005 Mail Address: salbertode@yahoo.com Verbs come in t...
-
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA(FREMU) BAINA YA …………………………………………….. S.L.P ………….., -TANZANIA. Ambaye katika mkataba ...
-
HISTORY NOTES FOR FORM FOUR & FORM THREE New Syllabus 2010 Prepared By: Sir. Alberto De Safari Mail Address: salbe...
No comments:
Post a Comment